Tuesday, December 10, 2013

UJUE UTAMU WA MAPENZI NA NAMNA YA KUJILINDA KWA UMPENDAE

 Kuna sababu za msingi kabisa kuelezea mambo ya kuzingatia ili kutambua vitu vitakavyokufanya ufurahie utamu wa ndoa yako. Kuishi na mke au mume sii kitu rahisi kama ambavyo watu wengi ambao hawako katika ndoa hufikiria. Hivi ni vipengere baadhi tu, wanandoa na wampenzi wanapaswa kuvitambua;

Kwanza kabisa ni kwambie kwamba utamu wa mapenzi sii lazima ufanye tendo la ndoa ama ngono, kuna mambo kibao ambayo moyo wa binadamu ukiyakosa huweza kukonda kama muathirika wa magonjwa hatari ya mwili. #"Upendo kutoka kwa yule umpendae", hili ndilo jambo kubwa la kwanza katika afya ya moyo ulio katika dimbwi la mapenzi.

Hakuna kitu kitamu kama kupendwa na ukapenda pia, kitendo hiki hufunga macho yote ya vishawishi vya dunia hii ya kidigitali. Usilazimishe upendo kwa mtu ambae unaonekana kuwa wewe tu ndiye unaye mjali wakati yeye hana habari na wewe. Ndio maana ukitaka kuingia katika ndoa lazima umtafute mtu unayempenda na anayekupenda ili muishi katika maisha yasiyo ya kushawishika kufuata matamanio mengine nje ya ndoa.

Kitu cha pili katika kufurahia utamu wa penzi ni #"amani" watu wengi wana wanaume na wanawake warembo, lakini hawafurahii mapenzi kwasababu hawana amani ndani ya nyumba. Utafurahia utamu wa mahusiano ya ndoa endapo utakuwa na moyo uliopondeka mbele za Mwenyezi Mungu, yani kuvumiliana katika changamoto za maisha.

Wapo watu wao ni maarufu kwa kuharibu mahusiano ya watu "tofauti na ndugu yako wa karibu" hakuna mtu anayefurahia kukuona unamwanamke mrembo ndani ya nyumba au mwanaume mtanashati ndani ya nyumba, na kwambia hili, jifunze kutunza siri za uzuri wa mkeo au mmeo. Kunawatu wanavitaka vitu hivi sana hata kwa gharama yoyote ile na popote vitakapopatikana vitanakuwa halali yao.

Kama mpenzi wako anakupa penzi tamu na la kistaarabu, basi haina haja ya kumueleza rafiki yako maana hujui yeye anakosa nini katika mahusiano yake na mwenzi wake. Pesa ni silaha kubwa sana katika mapenzi haya ya kizazi cha digitali, pesa zimekuwa na ushawishi mkubwa sana katika mapenzi hivyo unapaswa kuwa msiri katika mambo yako ya chumbani.

Cha msingi zaidi, hakuna mtu anayefurahi kusalitiwa katika mapenzi, kila mtu anatamani kummiriki mwenzi wake asipate wazo la kutoka nje ya mahusiano. Tunajua kabisa dunia hii kila siku tunakutana na wasichana warembo kabisa na pia tunakutana na wanaume watanashati sii kidogo, lakini kitu cha msingi ni kuyashinda macho na kuamini #"UKIONA VYAELEA UJUE............? Tukutane katika makala inayofuata.

KARIBU "ULIKE" UKURASA WETU WA FACEBOOK BONYEZA HAPA "MWANAHARAKATI"
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

News Update :
 
Copyright © 2013. Gsmmbaga@gmail.com - All Rights Reserved
Author: charlie | Powered by: .
Designed by: Mmbaga
^