Siku maji yakuoga niliyoletewa na mama mkwe yalivyobadilika na kuwa nyoka
Maisha yalizidi kunichapa na hatimaye sikuwa na namna zaidi ya kukimbilia kuolewa ili nimpate mwenza wa kusaidiana naye katika kuyakabili makali ya maisha.
Hebu fikiri mabinti wenzio umemaliza nao mwaka mmoja chuo na hata miaka miwili haijapita eti wanamilili biashara nzuri, pesa za kutosha, nyumba zao binafsi na kubadili magari kama miswaki kila kukicha na mwenzangu na mie hata fedha ya kununulia pad bado changamoto.
Kijana huyu nilikutana nae usiku mmoja katika night club mmoja maarufu iliyopo mkoani Mbeya na uhusiano wetu baada ya hapo ukatufungulia ukurasa mpya na kuamua kuoana.
Mwaka mmoja baadae tulioana kwa harusi iliyohudhuriwa na watu wengi na nashukuru maisha yakaanza salama huku tukiwa na furaha tele.
Familia ya kijana ilikuwa na mali nyingi sana na walikuwa wakijiweza sana pale wilayani mwao.
Nilipata mimba ya kwanza na mtoto alifia tumboni nami sikuwa na lakufanya zaidi ya kumshukuru Mungu kwani niliamini ni kwa mapenzi yake.
Mimba ya pili nilifanikiwa kujifungua salama na kumkuza mtoto ingawa alizaziliwa akiwa kama tahaira na kufa mwaka mmoja baadae kwa kifo cha kuungua na maji ya moto ambacho kilikuwa kama maigizo.
Nililia sana na kuomboleza kwa muda mrefu kabla kulia zaidi baada ya mimba ya tatu kutoka miezi michache kabla ya kujifungua.
Kichwani nikaanza kuhisi kitu na kuamua kumuuliza mwenzangu bila ya kuwa na majibu sahihi kutoka kwa mwenzangu nikaona hapa kuna jambo nikazidi kusali sana.
Siku moja mchana majira ya saa saba alikuja mama mkwe na mme wangu wakiwa wameshika ndoo yenye maji na kusema kuwa natakiwa kuyaogea maji yale kwani mimi nimepatwa na mikosi ya kwetu na ndio maana kila mimba inakuwa na matatizo.
Niliwakubalia muda ule na baada ya kuondoka nikayachukua maji yale mpaka kwa mchungaji wa kanisa langu ambaye alikuwa akinipa maombi maalumu na kuwaita baadhi ya waumini wenzangu na kuanza kiyaombea yale maji.
Kadri tulivyozidi kuomba maji yale yalizidi pia kubadilika na kuwa mazito na rangi ya ajabu kabla ya kugeuka na kutokea kitu cha ajabu kilichokuwa kikitoa sauti za kuzungumza kama binadamu kikisema, " kwa nini unatufanyia hivi? Si mme wako na mkwe wametuomba tukumaalizie kwani kosa letu nini?"
Mchungaji alizidi kuyaombea kabla ya kubadilika kuwa joka kubwa na kuteketezwa kwa moto uliowashwa na mchungaji mbele yetu.
Niliporudi nyumbani mama mkwe alikuwa mkali akidai kwa nini namtumia vichomi? Wakati nashangaa na mme wangu pia akawa kimya kama kalowa na maji na kuanza kuniomba msamaa kuwa mimba zote zile wao ndio walihusika kuzitoa ili tupate utajiri zaidi na sasa walitaka nipooze mwili wangu.
Niondoka na kurudi kwetu na baada ya miaka kadhaa nikiomba nimebahatika kuolewa na kubahatika kupata mtoto wa kiume mwenye miaka mitano sasa na mme wangu wa sasa ni mcha Mungu na tunaishi kwa amani, na wale mabinti waliokuwa na fedha sasa wote wapo jela kwani walikuwa wakijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.
Funzo
Wengi wetu hupotea kwa kutaka kujilinganisha na maisha ya wenzetu bila kujua wao wanaishije na mwishowe kujikuta tunaingia njia mbovu zenye majuto.
Maamuzi yangu ya haraka yangenipeleka kaburini
Je wewe umeshawahi jutia maamuzi yako?
Kuwa mfano wa kuigwa mafanikio mazuri hayaji kwa maamuzi ya kukurupuka
Ruksa kushare kama umeelewa
Fuata link YETU KUJIUNGA NASI kusoma maoni
0 comments:
Post a Comment