HESABU MAKOSA HAYA 7, HAKIKISHA HUYAFANYI KATIKA UHUSIANO WAKO - 7
Yapo makosa mengi ambayo watu huyafanya katika uhusiano. Katika mfululizo wa yale saba ambayo nilianza kuyachambua takriban wiki sita zilizopita, wiki iliyopita nilieleza kosa la Kukosea Tafsiri.
Angalia sana ndugu yangu, unaweza kuaibika kwa sababu ya tafsiri. Mwenzako anakusalimia kwa uchangamfu, badala ya kuchukulia kwamba hali inatokana na namna mnavyoheshimiana, wewe unachukulia kwamba anakuogopa. Endelea kusoma makosa mengine;
KUTARAJI UHUSIANO UKUPE FURAHA PEKEE
NI vizuri kutaraji furaha kwenye uhusiano wako, kwani ndivyo inavyotakiwa. Kosa linalojitokeza hapo ni kuwa wahusika huwa hawapigi mahesabu ya changamoto ambazo hujitokeza. Ni vizuri kuyabeba mapenzi katika sura halisi kwa maana zipo siku ambazo hutafurahi. Ni changamoto.
Tatizo ni kwamba kila mmoja anapoyatafakari mapenzi, huwaza kuwa mpenzi wake ndiye atayabadilisha maisha yake na kumfanya awe na furaha. Hata siku moja hawezi kwenda mbele na kuutesa ubongo wake, akiwaza na kuwazua jinsi ambayo yeye anaweza kufanya ili kumpa furaha na amani mwenzi wake.
Angalau wanaume wachache hufikiria mema kwa ajili ya wapenzi wao lakini kwa wanawake, tafiti zinaonesha kwamba asilimia 98 ya wanawake kabla ya kuingia kwenye uhusiano, husumbuliwa na ubinafsi kwa sababu huwaza mambo ambayo wao watafanyiwa na wapenzi wao na siyo wao kuwafanyia.
Kwa kuweka hoja zote kwenye kapu moja, ni vizuri kila mmoja akawekeza furaha yake kwa mwenzi wake. Ni makosa makubwa kutegemea matunda ambayo hujafanya jitihada zozote kuyapanda na kuyastawisha.

UBINAFSI
Katika maisha yako ya uhusiano, jiepushe na ubifsi. Wapenzi wanagombana, ndoa zinavunjika na familia nyingi zipo kwenye msoto kwa sababu ya ubinafsi. Tunazungumza mengi lakini ukweli ni kwamba endapo kila mmoja atafanikiwa kuushinda ubinafsi, upendo utashamiri kila kona.
Ubinafsi una matawi mengi. Mtu anaposaliti, maana yake ametekwa na tamaa binafsi. Anashindwa kutambua kwamba yeye ni mpenzi wa mtu, kwa hiyo anatakiwa kulinda penzi la mwenzake. Hajui kama anachokifanya ni dhuluma ya hali ya juu.
Ukweli ni kwamba unapoanzisha uhusiano na mtu, maana yake umeamua kumchagua yeye ndiye anamiliki penzi lako. Kwa hiyo ukienda kulitoa kwa mwingine, huo ni ubinafsi. Umeingiwa na umimi kwa kuona kwamba unatoa rasilimali za ndani ya mwili wako mwenyewe.
Kwa nini ukimfumania mwenzi wako panachimbika? Ni kwa sababu alichokitoa kwa mtu mwingine ni chako, kwa maana hiyo amekutendea dhuluma. Ndiyo maana ukawa na jeuri ya kupigana kwa sababu haki yako imetumika ndivyo sivyo.
Hivyo basi, usaliti ni ubinafsi. Umeingiwa na jeuri kwamba unacho ndani ya mwili wako, kwa hiyo unaweza kukitumia bila kumshirikisha mwenzi wako. Hiyo ni tabia mbaya mno. Kabla ya kusaliti, fikiria utakavyoumia pindi utakaposalitiwa.
Kama inauma, ni kwa nini umtende mwenzako? Je, umemuona yeye hana moyo? Anza leo kukemea ubinafsi. Popote pale utakapoona unachukua nafasi, upinge kwa sababu ni adui mkubwa mno kwenye mapenzi. Siku zote usiseme “nipo”, sema “tupo”.
Unapozunguka, usiwaze “upo”, unatakiwa kuwaza “mpo”. Hii itakusaidia kulinda siti ya mwenzako kila utakapokwenda. Hakikisha nafasi ya mwenzi wako haichafuliwi au kutolewa mkopo. Kama ilivyo kwenye soka, wachezaji huchezea timu nyingine kwa mkopo ndivyo na mapenzi ya sasa yalivyo.
Ni kweli mtu ana mpenzi wake lakini anavyojieleza anatoa picha kwa muulizaji kuona kwamba aliyepo si muhimu sana. Hii husababisha muulizaji aombe kukaa na baadaye hukaribishwa. Wengi walikaribishwa kwa mkopo, mwisho wakawa wamiliki wa jumla.
Kwa nini umwambie huyo mtu kwamba anaweza kukaa, wakati unajua siti ina mmiliki wake halali? Kwa porojo za kitoto, eti mnaambiana mfanye siri. Kinachosikitisha ni kwamba ukisikia na mwenzako naye kagawa siti yako kwa mwingine, macho yatakutoka kwa hasira.
Si wakati wa kuchukia unapotendwa, bali unatakiwa uache ubinafsi. Haliitwi penzi bila kuwepo watu wawili. Lazima uhakikishe unalinda la mwenzako ili na lako lilindwe. Somo la mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, linafundisha kuacha ubinafsi. Mfikirie mwingine.
Kama ambavyo ubinafsi unavyowatesa wananchi pale kiongozi mwenye dhamana kiserikali anaposhindwa kutimiza majukumu yake na kuamua kushughulikia shida zake binafsi, huku akitumia rasilimali za umma, ni kirusi hatari kila upande.

0 comments:
Post a Comment