JE UNAJUA BINADAMU ANATAKIWA KULALA MASAA MANGAPI?...
Unafikili ni wazo zuri kuamka saa 11 za asubuhi na kufanya mazoezi? Je, ingekuwa vipi kama ungetumia muda huo kulala?
Wataalamu wa afya wanashauri kuwa binadamu kwa kwaida anapaswa kulala angalau masaa 7 wakati wa usiku ili kuupa mwili afya bora.
Kulala kwa muda mfupi au masaa machache husababisha matatizo ya afya, ikiwa ni pamoja na shinikizo la damu, unyogovu, ugonjwa wa kisukari, na kupunguzwa kinga kukabiliana na chanjo.
Ni vyema ukatumia muda wako vizuri mchana ili usiku ukapata muda mwafaka wa kuweza kuupumzisha mwili ili kuepukana na magonjwa hatari ya shinikizo la damu, kisukari na kupungua kwa kinga mwilini.
Najua mazingira yetu waafrika ya kimaisha wakati mwingine yanachangamoto nyingi, lakini pale upatapo mwanya kidogo tu, basi utumie yani "kila penye tundu, penyeza lupia" au wawenzetu wazungu wanasema "one chance two goals".
0 comments:
Post a Comment