Friday, January 3, 2014

UMUHIMU WA MAZOEZI WAKATI WA UJAUZITO


Kufanya mazoezi wakati wa ujauzito kuna
umuhimu mkubwa kwa afya ya mama
mjamzito mwenyewe na mtoto wake
ambaye bado hajazaliwa. Wanawake wengi
wanatambua umuhimu wa kula lishe bora,
kuhudhuria kliniki, kuacha kuvuta sigara na
kunywa pombe wakati wakiwa na mimba.

Lakini si wanawake wengi wanaoelewa
umuhimu wa kutumia muda wao kufanya
mazoezi wakati wa ujauzito. Mazoezi yana
umuhimu mkubwa kiafya wakati wa
ujauzito kama ilivyo kabla ya ujauzito.
Kufanya mazoezi wakati unapobeba mimba
kunaleta faida kubwa wakati wa
kujifungua. Wakati wa ujauzito ni muhimu
kudhibiti ongezeko la uzito wa mama.
 
Kwa
kujishughulisha mama mjamzito na kuwa
na harakati humsaidia awe na afya bora na
kumsaidia aweze kupitisha kipindi cha
uchungu na kujifungua kwa urahisi zaidi.
Zaidi ya kumsaidia mama asiongeze uzito
mkubwa wakati wa mimba, kufanya
mazoezi humsaidia mama pia kurejea
katika uzito wake wa kawaida kwa urahisi
baada ya kujifungua kwa kawaida au kwa
uparesheni.

Kwa ujumla mama mjamzito
kama ambayo anavyoshauri kula chakula
bora na kuwa na afya nzuri wakati wa
ujauzito, hivyo hivyo hushauriwa pia
kuzingatia suala zima la kufanya mazoezi na
kuchunga mwili wake usiongeze uzito
mkubwa.
 
Pia kufanya mazoezi huufanya
mwili utoe mada ya endorphins, ambayo
husaidia kumfanya mama asipate matatizo
ya kifikra na msongamano wa mawazo
(emotional stress na depression).
Zifuatazo ni faida anazozipata mama
mjamzito iwapo atafanya mazoezi:

1. Mazoezi hupunguza maumivu ya
kichwa, kukosa choo na kuvimba mwili.
2. Mazoezi huongeza nguvu na kuupa
mwili stamina.

3. Mazoezi hukufanya ujisikie vizuri na
kukufanya uwe katika hali ya furaha.

4. Mazoezi hupunguza maumivu ya
mgongo na huimarisha mifupa ya
mgongo, makalio na mapaja na kuifanya
iwe na uwezo wa kuvumulia vyema uzito
wa mimba.

5. Mazoezi husaidia huongeza mtiririko
wa damu na hewa katika ngozi na
kuifanya ngozi yako ionekane nzuri.

6. Mazoezi hutayarisha mwili wako uwe
tayari kwa ajili ya kuhisi uchungu kwa
muda mfupi na kujifungua kwa urahisi.

7. Mazoezi hufanya mwili wako urudi
upesi katika muonekano wake wa
kawaida baada ya kujifungua.

8. Mazoezi humsaidia mama mjamzito
apate usingizi kwa wepesi na kulala
vyema.

Hata hivyo mama majamzito anashauriwa
kabla ya kuanza kufanya mazoezi apate
ushauri wa daktari na kuhakikisha kuwa
hana matatizo ambayo kwa kufanya
mazoezi pengine yakahatarisha mimba
yake.

Kwa wale waliokuwa wakifanya
mazoezi kabla ya kubeba mimba
wanashauriwa kuendelea na mazoezi yao
lakini kwa kuwa waangalifu na kwa
kiwango kidogo. Lakini kwa wale ambao
walikuwa hawafanyi mazoezi
hawaruhusiwi kufanya aina zote za
mazoezi wakati wa ujauzito. Mazoezi kama
vile kuogelea (kwa wale anaojua kuogelea),
kutembea na yoga ni miongoni mwa
mazoezi yanayoshauriwa wakati wa
ujauzito.
La muhimu ni mama mjamzito
kutokaa tu na kujiepusha na uvivu na
pengine kwa kufanya shughuli zake tu za
kawaida ambazo mama huwa anazifanya
nyumbani kila siku ikawa inatosha kuwa
mazoezi yake na akaongeza kwa kutembea
kidogo ( walking) kila jioni.
 
Kutembea ni
mazoezi salama na rahisi kwa kila mama
mjamzito na yanayojulikana na kila mtu na
kuweza kufanywa mahala popote. Ni bora
kama unaweza fanya mazoezi na mwenza
wako, rafiki au hata ndugu na jamaa yako
ili uweze kufurahia zaidi mazoezi hayo.
Pia
muhimu ni kufuata maelekezo ya daktari
kwani si kila mama mjamzito anaruhusiwa
kufanya mazoezi wakati wa ujauzito
kutokana na sababu tofauti. Baadhi ya
mazoezi ambayo yana madhara kwa afya ya
mama mjamzito na kwa mtoto
hayaruhusiwi kabisa kufanywa wakati wa
ujauzito.
Mazoezi hayo ni kama vile mazoezi
ya aerobic, ski, kupanda mawe, kupanda
farasi na mengineyo kama hayo. Iwapo
unaishi katika miji iliyoendelea basi
unaweza kupata kwa urahisi vituo maalum
kwa ajili ya kufanyia mazoezi mama
wajawazito, na katika vituo hivyo kwa
kawaida wakina mama wajawazito
hukusanyika na kufanya mazoezi kwa
pamoja. Lakini kama uko katika miji
ambayo vituo hivyo hakuna usife moyo, na
jitahidi kufanya mazoezi hayo peke yako
huku ukishirikiana na familia yako.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

News Update :
 
Copyright © 2013. Gsmmbaga@gmail.com - All Rights Reserved
Author: charlie | Powered by: .
Designed by: Mmbaga
^