Sunday, December 8, 2013

MIAKA IJAYO MAHOUSE GIRL NDIO WATAKUWA WAKE WA KUOA...

Kama nilivyo elezea kwenye kichwa cha habari hapo juu,
siku hizi watu wengi wamekuwa na mtindo wa kuajiri wasichana wa kazi (mahouse girl) ili kusaidia kazi za nyumbani.
Ndio hatukatai pengine mama mwenye nyumba anaweza kuwa anazidiwa na kazi,
Kama kufua nguo za mzee,watoto,kunyoosha, kuandaa chakula nk.
Lakini kuna wadada/wanawake wengine unakuta watu wako wawili yeye na mumewe,
eti nao wanaweka house girl sijui wa nini?eeh!!!
tena wengine sijui ni sifa eti anaajiri wawili kabisa kwa kazi zipi sasa?na wewe ufanye kazi gani?
Ya kupaka rangi kucha na kuchat kwenye mitandao? halafu bila aibu unasifia chakula alichoandaa house girl mbele ya mumeo.



Na unaangalia tu house girl anamnawisha mikono mumeo na kumkausha na taulo,wewe upo tu kwenye kiti kama umegundishwa na super glue vile.
huyo jamaa yako akila chakula kitamu cha house girl, si atataka ale na kile cha usiku aone utam wake?
hapo ndipo timing zinapoanzia na ukizingatia mahouse girl walivyo na heshima,
baba akifika na kamzigo anapokelewa kwa mikono miwili na anapigiwa goti,
wakati huo we upo upo tu kama koti la mvua linasubiri masika.
Sijui ndio kusema hamuelewi mko pale kwa ajiri gani?na house girl akiboronga kidogo tu macho na sauti ya ukali inakutoka kama nini,
Hujui kwamba unapofanya hivyo unamkomaza house girl,hapo kwako ni sawa na chuoni kwake anachukua mafunzo ya maisha.
Mumeo akisifiwa kazini nguo zake zinang'aa atamkumbuka house girl,
akisifiwa kwamba ananawili atamkumbuka house girl,
akisifiwa kwamba viatu vyake vinang'aa atamkumbuka house girl,
Ndio si house girl ndio anaye fanikisha yote hayo?wakati wewe uko bizy ku up load picha fb?
mwisho wa siku unatemwa kama big G iliyo chacha,
halafu watu wanabaki kushangaa mbona jamaa kamuacha mwanamke mzuri vile halafu kabeba house girl?
kumbe ni janga la kitaifa hajui A wala B kifupi hajitambui,
Badilikeni nyie kina Eva ma house girl watawapiga bao ohooo!!!!!!
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

News Update :
 
Copyright © 2013. Gsmmbaga@gmail.com - All Rights Reserved
Author: charlie | Powered by: .
Designed by: Mmbaga
^