YATAMBUE MADHARA YA KUFANYA NGONO MARA KWA MARA..
Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi,
lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo
huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono.
Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku
wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.
Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia
‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya
kufanya hivyo kwa sababu amelipa mahari.
Hilo linaweza kuwa
jambo jema kwa upande mwingine, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati
ya watu wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu
wapenda ngono.
Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo
mtu asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni
vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika
kufanya mapenzi kila tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya miti
kwa vile tu miili imetaka kufurahika.
Twende pamoja katika kutazama madhara hayo kwa kina.
KUPOTEZA HAMU YA TENDO.
Watu wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za
kimapenzi kwa wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza
kujitokeza wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara.
Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea
mwenza kiasi cha kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu.
Aidha kukinai haraka staili za kimapenzi kunatajwa
kujitokeza kutokana na kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na
pengine sehemu moja, kitanda kimoja na chumba kile kile, jambo ambalo linaweza
kumfanya mhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo kupoteza hamu naye
na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.
KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA.
Tabia ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji
wa homoni mwilini na kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa
kwa tendo la ndoa bila kukosa na hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo
wa kuzuia tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi na kwa wakati
gani?
Watu wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara
ndiyo wale ambao kila wanayemtazama barabarani humtamani bila kujali hadhi
yake.
Hawa ndiyo
wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata kwa watumishi wa ndani au kufanya mapenzi na
watoto wao wa kuwazaa kwa vile akili zao huwa zimeathirika kwa tamaa ya
mapenzi.
Unapokuwa mtu wa
kufanya mapenzi mara kwa mara huwezi kuwa na uwezo wa kuzuia tamaa yako. Mumeo
akiondoka siku mbili unatamani kuwa hata na houseboy ili akukate kiu ya
penzi.
KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO.
Raha ya tendo hutegemea sana hisia iliyokuzwa kutokana na
mapenzi sahihi na kiu ya kufanya mapenzi, hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya
mapenzi kila mara unaweza kupoteza msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha
ambayo haikutoshi kumaliza tamaa yako.
Kama ni mapenzi
utakuwa unayafanya kwa mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo!
KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI.
Madhara mengine yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi
mara kwa mara ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili.
Kama tujuavyo tendo
la ndoa hasa kwa wanaume huwafanya watumie nguvu nyingi, hivyo kuufanya mwili
uchoke. Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa wafanya mapenzi mwili hukosa nguvu za
kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha.
Sambamba na hilo mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume
wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa dhaifu.
KUPATA MAGONJWA.
Kama tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya mapenzi mara kwa
mara huwa na tamaa na hujikuta wanafanya mapenzi holela ambayo huweza
kuwasababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi, lakini ufanyaji wa mapenzi
usiokuwa na msukumo wa kutosha hasa kwa wanawake huwafanya waishiwe msisimko na
kuzifanya sehemu zao za siri kutotoa ute unaoweza kuwakinga na michubuko wakati
wa kujamiiana na hivyo kuwasababishia michubuko itakayoweza kuleta maambukizi ya
haraka ya magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi
0 comments:
Post a Comment